Mwanariatha Copro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza
mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano
yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’
yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi
1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na
kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City
Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/=
ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga
kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
MWANARIADHA mahiri Copiro
Mwita wa Mwanza na Mary Naaly wa Arusha, jana waliibuka vinara upande wa
wanaume na wanawake, katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 ya ‘Rock City
Marathon 2012’ yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume akitumia saa
1:04:02, huku Mary akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa
1:16:33, katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wanariadha 497 waliokimbia
katika makundi matano.
Dotto Ikangaa kutoka Arusha aliibuka mshindi katika mbio za
kilometa tano wanaume, akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika
nafasi ya pili, huku Paul Elias kutota Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.
Rock City Marathon ni mbio zinazondaliwa na kampuni ya
Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa
na NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New
Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB).
Katika mbio hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa
na msanii maarufu wa Tanzania Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK
Wanaume, akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi
Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.
Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya
kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika
mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini
Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada
ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 497
walijitokeza kushiriki mashindano hayo.