BONGO MUVI

MUONEKANO MPYA WA JACQULINE WOLPER






MARIOVAN PEEBLES KUZINDUA FILAM YAKE MLIMANI CITY
Wakazi wa Dar es Salaam watanufaika na ujio wa muigizaji na muongozaji wa filamu wa Hollywood Mario Van Peebles aliyealikwa mwaka huu kama mgeni wa heshima kwenye tamasha la filamu la kimataifa Zanzibar, ZIFF.Van Peebles ataizindua filamu yake ya mwaka huu iitwayo ‘We The Party’ ambayo ameiongoza na kuigiza pia.Kwa ushirikiano na ZIFF, kutafanyika ‘red carpet premier’ ya filamu ya ‘We the Party’ kwenye ukumbi wa Century Cinemax cinema wa Mlimani City.Tukio hilo litahudhuriwa na yeye mwenyewe Mario Van Peebles na mwanae wa kiume Mandela Van Peebles aliyeigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu hiyo.Filamu hiyo itaoneshwa kwa siku tano mfululizo ili kutoa muda zaidi kwa watu kuiona.We The Party iliyoigizwa jijini Los Angeles inahusisha marafiki watano wanafunzi wa high school wanaozungukwa na mapenzi, pesa, kujirusha, chuo, sex, bullies, Facebook na mambo mengine.

Rapper Snoop Dogg anaye ameigiza kwenye filamu hiyo.
Rose Ndauka atoka na sinema ya ‘Love Me or Love Me Not’
Msanii wa tasnia ya Filamu Bongo, Rose Ndauka anatarajia kuja na muvi yake ya kwanza kabisa ambayo ameifanya na kampuni yake binafsi inayoitwa Ndauka Entertainment ambayo ndio imesimamia mpango mzima wa utayarishaji na utengenezaji wa muvi hiyo.
Akizungumza na Bongo5 Rose Ndauka alisema muvi hiyo inaitwa “Love Me” na kwamba maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni muvi hiyo kuingia sokoni.
Akiendelea alisema “muvi yangu inatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi mwezi wa sita ambapo itatoka chini ya usimamizi na usambazaji wa kampuni ya Pili Pili Entertainment. Rose aliwataja wasanii wengine walioshiriki katika Muvi hiyo kuwa ni pamoja na Irene Paul na Michael Rodriguez”.
Kuhusu ni wapi muvi hiyo imeshutiwa msanii huyo amesema Muvi yote imefanyika ndani ya Jiji la Dar-Es-Salaam. Amewaomba mashabiki kumpa sapoti pindi Muvi hiyo itakapotoka na kuwaambia kuwa wasubirie makubwa toka Ndauka Entertainment.


1 comment:

Anonymous said...

MUONEKANO UKO POA SANA.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...