Wednesday, October 31, 2012

NGOMA MPYA YA ‘NATAKA KULEWA’ YA DIAMOND, YADAIWA INAMHUSU ‘WEMA SEPETU’ KWA ASILIMIA MIA…!!

MSANII anayeshikilia nafasi ya juu kwa sasa kwenye muziki wa kizazi kipya Tanzania Nasseb Abdul ‘Diamond’, inasemekana kuwa ameamua kutoa ya moyoni juu ya  Wema Sepetu katika ngoma yake mpya ya ‘Nataka Kulewa’, ambayo imezungumzia matukio yote yaliyomkuta alipokuwa na mwanadada huyo na mengine ambayo yalikuwa yanazungumzwa na watu pindi wakiwa wapenzi.

Chanzo kimoja cha karibu na msanii huyo kilizungumza na DarTalk, kilidai kuwa mistari yote inayopatikana ndani ya ngoma hiyo ni matukio ambayo Diamond alikuwa ameyafanya kwa Wema na mengine ya kusikitisha ambayo awali yalikuwa yanazungumzwa na yeye alijua uzushi.

Tuesday, October 30, 2012

MWITA NA NAALI WANG;ARA MBIO ZA ROCK CITY MARATHON 2012

 Mwanariatha Copro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.

Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
MWANARIADHA  mahiri Copiro Mwita wa Mwanza na Mary Naaly wa Arusha, jana waliibuka vinara upande wa wanaume na wanawake, katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 ya ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume akitumia saa 1:04:02, huku Mary akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa 1:16:33, katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wanariadha 497 waliokimbia katika makundi matano.
Dotto Ikangaa kutoka Arusha aliibuka mshindi katika mbio za kilometa tano wanaume, akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili, huku Paul Elias kutota Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.
Rock City Marathon ni mbio zinazondaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa na NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Katika mbio hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa na msanii maarufu wa Tanzania Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK Wanaume, akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.
Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 497 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.

TAZAMA SHOW YA AY-NA CP BILCANAS

 Feza Kessy na Ay...
 Cpwaa
 Chidi kwenye Interview

 Cp kwa Stage
Dancers wa Cp

RAY AWAJIBU WANAOONGEA SANA JUU YA YEYE KUTOFANYA FILAMU KIMATAIFA…!!

MSANII mahiri wa filamu Tanzania anayeaminika kuwa anastahili kufanya kazi kimataifa kutokana na uwezo wake Vicent Kigosi ‘Ray’, amefunguka na kuwajibu watu wanaokaa kila siku na kumtaka afanye filamu hizo, kuwa yeye hajutii kutofanya kazi hizo kwani anazofanya zinamtosha na si lazima yeye kufanya kazi hizo.

Wapo baadhi ya wasanii wanaoamini kuwa
Ray ana uwezo mkubwa kisanaa wa kufanya filamu na wasanii wa nje lakini wanashindwa kuelewa kwa nini karidhika na umaarufu wa ndani wakati uwezo wake ni mkubwa.

Monday, October 29, 2012

MASHINDANO YA KAULI-MBIU - TUMWAMINI YUPI ???


HOTUBA HII YA WAZIRI MALUGO NI AIBU

NAIBU Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Augustino Mulugo amefunguka kuwaomba radhi Watanzania kwa kujichanganya kwake katika hotuba aliyoisoma kwenye mkutano wa kimataifa nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
Global Publishers

Sunday, October 28, 2012

UJIO MPYA WA DIAMOND PLATINUMZ UTAKUA HUU”NATAKA KULEWA(NIACHE)


AY NA CPWAA WAANZISHA KAMPENI MAALUM KWA AJILI YA KUPIGIWA KURA TUZO ZA CHANNEL O 2012

“WANAOSEMA NAONGOZA KWA KUIBA WANAUME ZA WATU NI WALE WENYE NIA YA KUNICHAFUA” – AGNES MASOGANGE…!!

MWANADADA anayejipatia umaarufu kupitia video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Agness Masogange, amefunguka nakusema hatumii mwili wake kama chombo cha kuwakamata wanaume bali hutoa penzi lake kwa yule anayempenda na ishu zinazozungumzwa mitaani kuwa anaongoza kwa kuiba wanaume za watu si kweli na wanaodai hivyo hawamtakii mema.

Saturday, October 27, 2012

JACKLINE WOLPER’ ANYAKUA TAJI LA ‘IJUMAA SEXIEST GIRL 2012′…!!


 Chidi Benz (Chuma) akitoa burudani
 Msanii Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki
MSANII wa filamu Bongo, Jackline Wolper, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl 2012 ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima. Usiku wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa
Ommy Dimpoz, Chidi Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.

MISS TALENT 2012 NDANI YA GIRAFFE HOTEL

 Mshiriki namba 17 kutoka Rukwa Vency Edward akionesha umahiri wake wakucheza
 Mshiriki namba 13kutoka kanda ya mashariki,Joyce Balui akionesha uwezo wake wakusakata dansi
 Mgeni rasmi katika onyesho la Red's Miss Talent alikua Mbunge wa viti maalum -Arusha (katikati)Mh-Catheline Magige akizungumza machache
 Mshiriki namba 27 kutoka Ilala,Noela Machael akionesha kipaji chake cha kuimba
 Mshiriki namba 30,Waridi Frank akionesha jinsi yakucheza ngoma za asili
 Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012 Baby Love kalala"kati kati"akiwa kwenye picha ya pamoja na warembo wengine
 Mshiriki namba 8 kutoka kanda ya ziwa Happy Rweyemamu akionesha kipaji chake chakuruka sarakasi
 Mshiriki namba 1 kutoka Kilimanjaro Nandi Rafael akionesha umahiriwake wakucheza dansi
 Mshiriki namba 29 kutoka Dodoma akioneza jinsi yakucheza Dansi
 Mshiriki namba 15 kutoka Temeke Catherine Msumbigana akionesha kipaji chake chakupiga zeze.
 Mshiriki namba 3 kutoka Chuo huria,Zuena Naseeb akionesha umahiriwake wa kuimba.
Mshindi wa Redd's miss Talent akionesha jinsi yakucheza ngoma za asili kwakutumia nyoka.

MATUKIO YA KIIMANI YAZIDI KUCHUKUA KASI

Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Arusha, Abdukarim Jonjo akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru akipata matibabu baada kujerehiwa na kitu kinachodhaniwa ni bomu juzi usiku na watu aliodai kuwa ni waumini wenzake. Picha na Filbert Rweyemamu

Friday, October 26, 2012

PICHA ,HEINEKEN ILIVYOSABABISHA UZINDUZI WA SKY FALL YA JAMES BOND.

 AY-na-Madam-Rita

 Master-Jay-akibadilishana-mawazo-na-mdau

 Nancy-Sumari-na-Shaa
 Sam-Misago
 Captain-G-naye-hakukosa
 Feza-Kessy-2

 Nancy-Sumari-na-Luca-Neghesti
 Sade-na-Jokate
 Watangazaji-kwenye-pozi
 Reuben-Ndege-na-Jokate
 Madam-Rita-akihojiwa-na-Capital-TV

 Sam-Misago-na-Shaa

 Dj-Fetty-na-marafiki-wakibadilishana-mawazo

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...