Monday, December 31, 2012

THIS IS DIAMOND; ANGALIA PICHA KWENYE Interview YA X-LIVE JANA KUHUSIANA NA USIKU WA WASAFI 1/1/2013 MAISHA CLUB....



Saturday, December 29, 2012

CATHERINE MASUMBIGANA NDIYE UNIQUE MODEL 2012

Hawa ndiowalioingia tano bora
Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.

 Washiriki walioingia tano bora

HUYU NDIO KIJANA ANAYE DAIWA KUCHOMWA MOTO NDANI YA NYUMBA YA JOSE CHAMELEON AKIWA HOSPITALINI MDA MFUPI KABLA YA KIFO CHAKE.

NYUMBA YA  JOSEE CHAMELEON

Monday, December 24, 2012



SIKILIZA WIMBO MPYA wa LORD EYES ft. BEN PAUL - NO MORE DRAMA

Saturday, December 22, 2012

TAJOA;MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAMPA DHAMANA LULU;Msanii Lulu kula Xmas akiwa kwao

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inadhaminika.

Kwa maana hiyo, Lulu sasa atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusudia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru

Friday, December 21, 2012

TAMTHILIA MPYA NA NZURI KUTOKA BONGO IITWAYO - HIGH HEELS,WAHUSIKA NI ,RAYUU,CHUZ,NA WENGINE KIBAO

 Mr.Chuz
 Mtunzi ni tuesday kihangala na mtaharishaji , Pia wasanii wa jumba la dhahabu utawakuta humo hii ni zaidi ya jumba la dhahabu
Rayuu

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2012 YATANGAZWA

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa leo ametangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2012 uliofanyika nchini kote  tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.   

Katika Mtihani huo Jumla ya wanafunzi 894,881 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambapo   wavulana ni  426,285 sawa na asilimia 47.64  na wasichana ni 468,596  sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya  wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379  ambao walitarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 walitarajiwa kufanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.  

Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39.  Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.


HUU NDIO MSIMU WA SIKUKUU BWANA,TAZAMA UMATIWA WATU WANAVYO ONEKANA STEND KUU YA MABASI"UBUNGO"WAKITAKA KUSAFIRI


Wednesday, December 19, 2012

TAZAMA THE PLATNUM "KESHO"

MAGAZETI YA LEO JUMATANO ,UDAKU,MICHEZO NA SIASA





Tuesday, December 18, 2012

TAZAMA MKASI S05E04 NA SUGU

CHEKI VIDEO MPYA "PREZZO NA CANIBAL MY CITY TOWN"

Monday, December 17, 2012

TAZAMA PICHA ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA LINAH-'USHAFAHAMU'




Thursday, December 13, 2012

TAZAMA PICHA , ETI INASEMEKANA HAWA WALIKATISHA KATIKA KAMBI YA JESHI! NAHII NDIO ATHABU YAO


MAKUBWA HAYA ANGALIA PICHA MIKE TYSON AJIGEUZA NA KUWA MWANAMKE!


Mmoja amesema kwamba: “Huko nyuma, alikuwa  anapenda sana kuvaa sana glovu za kike, viatu virefu vya ngozi vya kike na magauni ya hariri, na pia alikuwa ni mtu mwenye kupenda sana heleni.”
 Tyson ambaye amebadili jina na kujiita Michelle.
“Watu wanaona ni ajabu mie kuwa mwanamke hivi sasa,” alisema Tyson ambaye aliwahi kufungwa kwa kubaka, na ambaye amefanyiwa mabadilko kadhaa ya uso, pua na viungo vingine kwa masaa 16.  Aliongeza kwamba: “Hata nilipokuwa bondia nilikuwa natamani sana kuwa na matiti na nyeti za mwanamke.”Iron Mike au Iron Maiden kama anavyojulikana sasa aliyasema hayo akiwa ametulia huku amevaa wigi la kike, suruali ya ‘jeans’ ya bluu na T-shirt yenye picha ya Vanessa Bruno ambapo alidokeza kwamba mara sehemu zote nyeti za kike zitakapojitokeza atawadhihirishia Wamarekani kwamba yeye si “mvulana mbaya” tena.Amesema  ameutunza uume wake ulioondolewa katika chupa ili kuwakumbusha wabaya wake waliokuwa wakimfanyia  vitendo vya kuchukiza yeye na “wavulana wazuri” wengine huko gerezani.Japokuwa wachambuzi wa masuala ya ndondi mwanzoni walishangazwa na maneno hayo ya Tyson, wengi wamekiri kwamba alama za yeye kupenda hivyo zilikuwepo.

Mike Tyson 'Michelle' ambaye anayedaiwa kujibadili na kuwa mwanamke.
BINGWA mashuhuri wa zamani wa uzito wa juu duniani, Mike Tyson, anasemekana yuko katika hali nzuri baada ya kujibadili na kuwa mwanamke katika operesheni aliyofanyiwa huko Beverly Hills, Marekani, hivi karibuni ambapo amebadili jina na anajiita Michelle.

Kuna wakati Tyson alikuwa anajulikana kama “Mtu mwenye sura mbaya zaidi duniani”!

Tuesday, December 11, 2012

UWOYA ATOA KITUKO CHA MWAKA

Kituko hicho kilitokea katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wakati Uwoya alipokuwa akiomba kura mbele ya wasanii wenzake.

Kauli yake hiyo iliwashangaza wengi kwa kuwa Uwoya ni mmoja kati ya wasanii wanaoongoza kwa kuandikwa kwa skendo.
“Hakuna asiyejua jinsi skendo zilivyonichafua, nilipogundua kuwa zinaniharibia maisha nikaachana nazo, sasa ole wao wote wenye tabia za aina hiyo, hakika watanitambua,” alisema na kuzua minong’ono.
Pamoja na minong’ono hiyo, Uwoya alifanikiwa kuwabwaga wapinzani wake Benny Kinyaiya na Lissa Aidan na kuchukua nafasi hiyo.

RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE AMSAIDIA RAY C

Mh.Raisi Kikwete akiwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati mwanamuziki huyo alipoenda kumtembelea Raisi na kumpa shukrani kwa kumsaidia kwenye matibabu ya juu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Aidha Ray C alimueleza Raisi kwamba afya yake imeimarika na kwamba muda mfupi ujao atarudi kuendelea na kazi yake ya muziki. Kwa upande wa mama yake Ray C amemshukuru Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanae kwa kugharamia matibabu yote ya mwanae.
Raisi Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Ray C, Mama yake mzazi Ray C - Margreth Mtweve na aliyevaa nguo za pinki upande wa kulia ni dada yake Ray C - Sarah Mtweve.

Monday, December 10, 2012

TAZAMA PICHA YA KITUKO IKIMUONYESHA VAN PERSIE VS ROONEY WAKIWA WANAWACHAPA MAHATERS WOTE

This one for the HATERS.. We did beat the history (liverfools), we did beat the college staffs (Arsenal)... We made it against the fake champions of EUROPE (Chelsea)... Where are they ?? the so called Money spenders.. Shitty.. Haters, keep talking.. we'll keep winning.. hehee.. HapPy new Year EPL leaders!!

MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA UDAKU,SIASA NA MICHEZO


Sunday, December 9, 2012

WIKI HII NAWAACHA NA MSEMO HUU


TAZAMA SCENE YA MWISHO ALIYOCHEZA MAREHEMU SHARO MILIONEA NA KITALE

HAYA NDIYO YALIYOJIRI LEO KATIKA UWANJA WA UHURU KATIKA KUMBU KUMBU YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya  maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.

Saturday, December 8, 2012

TAZAMA PICHA JINSI GARI ILIVYO TUMBUKIA MTONI ENEO LA JANGWANI JIJINI DAR






Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...