MICHEZO


Mchezaji wa kiungo wa Mali Seydou Keita amekihama klabu cha Barcelona baada ya kukichezea kwa miaka minne.
Katika muda huo wa miaka minne, Keita aliisaidia Barcelona kuzoa jumla ya vikombe 14.
Wakati wakithibitisha kuondoka kwa mwamba huyo, Barca walimishukuru Seydou Keita kwa juhudi zake za kuletea klabu hicho cha Uhispania mafanikio na vile vile wakamtakia kila lakheri anakokwenda.
Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu kimoja cha Uchina, Dalian Aerbin
Ikiwa hatiamae ataishia China basi Keita hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Afrika kufanya hivyo.
Majuzi nahodha wa timu ya Ivory Coast Didier Drogba aliwafuata Frederic Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wa Nigeria kujiunga na timu za ligi kuu ya China.
Keita, mwenye umri wa 32, alijiunga na Barcelona mwaka 2008 kutoka Sevilla akiwa ni mchezaji wakwanza kabisa ambaye Pep Guardiola alimsajili mara tu alipochukuwa uongozi wa Barca.
Kabla ya hapo mchezaji huyo alikuwa Olympic Marseille, Lorient na Lens zote za Ufaransa na ndio baadaye akahima Seville ya Uhispania.
Keita amehama baada ya Guardiola luondoka kama Meneja wa Barcelona na mahali pake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake Tito Vilanova

Ferdinand atozwa faini

Rio Ferdinand
Beki wa Manchester United Rio Ferdinand ametozwa faini ya pauni za Uingereza 45,000 sawa na dola za kimarekani $71,000 na chama cha mpira cha England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha mbovu kuhusu beki wa Chelsea Ashley Cole.

Halmashauri huru imempata na hatia kwa kumkashifu Cole akitumia lugha inayopdhalilisha ukoo na kabila la mpinzani kwa msemo wa maneno 'Choc ice' kwa maana mtu mweusi nje na ndani mzungu.

Ferdinand alikanusha kua sivyo hivyo ila ni kwamba maanake ni mtu feki, au mnafiki.
Matamshi yaliyopeperushwa kwa mtandao wa Twitter yalitokea baada ya Ashley Cole kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mdogo wake Rio aliyedai kua alitukanwa na John Terry. Terry hakupatikana na hatia.

Ashley Cole



No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...