Tuesday, October 30, 2012

RAY AWAJIBU WANAOONGEA SANA JUU YA YEYE KUTOFANYA FILAMU KIMATAIFA…!!

MSANII mahiri wa filamu Tanzania anayeaminika kuwa anastahili kufanya kazi kimataifa kutokana na uwezo wake Vicent Kigosi ‘Ray’, amefunguka na kuwajibu watu wanaokaa kila siku na kumtaka afanye filamu hizo, kuwa yeye hajutii kutofanya kazi hizo kwani anazofanya zinamtosha na si lazima yeye kufanya kazi hizo.

Wapo baadhi ya wasanii wanaoamini kuwa
Ray ana uwezo mkubwa kisanaa wa kufanya filamu na wasanii wa nje lakini wanashindwa kuelewa kwa nini karidhika na umaarufu wa ndani wakati uwezo wake ni mkubwa.

Alisema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakitoa macho kwa msanii mmoja hasa yeye kuwa ndiyo anayeweza kufanya hivyo, lakini anashindwa kuelewa ni kwa nini wasijipe nafasi hiyo wao ili wafanye kwa faida zao na maisha yao.

“Hakuna msanii aliyeandikiwa kuwa atakuwa anafanya kazi za kimataifa, na kufanya hivyo ni jukumu la mtu mwenyewe pia si lazima hivyo wanaonitolea macho mimi kwa nini wao wanashindwa kufanya hivyo nahisi hawajiamini na kazi zao,”
alisema.

Aliongeza kuwa kila mtu katika maisha yake huwa anajiwekea malengo hivyo watu wanaweza kusema mtu fulani mbona afanyi vile lakini wanashindwa kuelewa kuwa kila jambo huja kwa mipango na si kukurupuka na kufanya na mwisho wake aibu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...