Tuesday, October 30, 2012

MWITA NA NAALI WANG;ARA MBIO ZA ROCK CITY MARATHON 2012

 Mwanariatha Copro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.

Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
MWANARIADHA  mahiri Copiro Mwita wa Mwanza na Mary Naaly wa Arusha, jana waliibuka vinara upande wa wanaume na wanawake, katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 ya ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume akitumia saa 1:04:02, huku Mary akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa 1:16:33, katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wanariadha 497 waliokimbia katika makundi matano.
Dotto Ikangaa kutoka Arusha aliibuka mshindi katika mbio za kilometa tano wanaume, akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili, huku Paul Elias kutota Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.
Rock City Marathon ni mbio zinazondaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa na NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Katika mbio hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa na msanii maarufu wa Tanzania Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK Wanaume, akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.
Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 497 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...