Wajumbe wa Baraza la Wiki
ya Nenda kwa Usalama wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha ziara
yao ya kutembelea mliama Kitonga. Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa
Usalama kitaifa yanafanyika Mkoani Iringa
Lori la mizigo lililosheheni mbao likiteremka mlima Kitonga hii leo.
Askari wa Usalama barabarani wametakiwa kuongeza doria katika mlima huo kufuatia ajali za mara kwa mara zinazotokea kutoka na madereva kuendesha kwa fujo bila kuzingatia usalama barabarani.
Mteremko wa Mlima Kitonga
Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani leo wametembelea
maeneo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea ajali mara kwa mara katika barabara
kuu ya Morogoro-Iringa-Mbeya na kupeana ushauri juu ya hatua za kuchukua katika
kupunguza ajali hizo.
Pichani ni Kamanda wa Trafiki Mkoa wa Iringa, Mrakibu wa Polisi
Pamphil Honono akiwaonesha wajumbe hao maeneo hayo wakati wamesimama katika
kijiji cha Lugalo mkoani Iringa ambako ndio kuna kona ya mwisha ya Mlima
kitonga. Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalkama Kitaifa yanafanyika mkoani
Iringa na Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA
BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
No comments:
Post a Comment