MSANII
wa filamu ambaye ameamua kuigia upande wa pili wa muziki, Snura,
amesema hahitaji kuonekana anafanya show bali malengo yake ni kuleta
mapinduzi katika muziki huo na suala nzima la kitawala stage ili azidi kujiweka
tofauti na wengine.
Msanii huyo alisema wasanii wengi wa Tanzania ni wavivu kwenye kutawala stage kwani mara zote huwa wanasimama sehemu moja kutokana na uvivu huku hata kucheza wanashindwa kutokana kujiona na wengine wanawatumia sana wacheza show wao.

Msanii huyo alidai kuwa ameamua kufanya
muziki basi hawezi kutoa ngoma nyepesi nyepesi kwani anamini watanzania
wanataka kuona nini anachokifanya, huku mapingo yake katika muziki huo ni
kuonesha kazi kama wasanii wa nje ambao wanafanya muziki kwa kujituma na
si kujionesha kama baadhi wa hapa bongo.
“Tazama wasanii wengi wa bongo kwenye suala la kucheza wao ni wavivu, hivyo kwa upande wanu sihitaji kuwa kama wao na ndiyo maana nafanya mazoezi ya kutosha kwani naelewa muziki unataka nini na watu wangu wanataka nini kwa wakati gani,” alisema.
Aliongeza “kwa wale wabaya wangu hata kama wakizidi kuniombea mabaya hawawezi kunipata kwani ‘dua la kuku halimpati mwewe’ na kwa njia hiyo nitazidi kuchanua na kufika mbali zaidi.”

No comments:
Post a Comment