WAKATI wadau wa filamu na kazi
za wasanii wakimtolea macho Aunty Ezekiel, baada ya picha zake za
nusu uchi kusambaa huku zikidaiwa zinavunja maandali ya kitanzania, msanii Salma Jabu ‘Nisha’, amezitolea uvivu picha hizo na kudai kuwa endapo angekuwa na
madaraka juu ya BASATA basi angechukua hatua za kumfungia haraka msanii huyo
kwa muda.
“Ingekuwawa mimi nipo kwenye
uongozi wa juu wa BASATA ningetoa mfano mkubwa ili wasanii wengine wasifanye upuuzi
kama huu, unajua kuna watu wakiona wapo kimya wanatafuta visababu vya kijinga
ili tu watu wamzungumzie lakini si kwa ishu hii kwani hapa anajiumiza
mwenyewe,”alisema.
Hata aliongeza tabia kama hizi zikiendelea kwa
wasanii basi tasnia nzima ya filamu itaendelea kuchukuliwa ni ya wahuni,
na heshima itapungua sana hata kama wengine wakiwa na si wavunjaji
wa maandali ya kitanzania.
Alisema kuwa yapo mambo ambayo msanii anaweza
kuyafanya jukwaani mbele ya mashabiki, lakini si kuvua nguo hadharani na
kuacha mwili wako ukiwa hauna kitu, kwani ni kitu ambacho kinaleta picha
chafu kwa watanzania na hata wadau wengine wanaoishi nje.
No comments:
Post a Comment