Friday, September 21, 2012

FILAM MPYA YA STIVEN KANUMBA,BAADA YA MIEZI SITA YA KIFO CHAKE

Kwa mara ya kwanza toka kifo chake April 7 mwaka huu filamu mpya ya Marehemu 'Steven Charles Kanumba' inatarajiwa kuingizwa sokoni na kampuni ya usambazaji ya Step Entertainment ya hapa nchini. Filamu hiyo itakayokuwa ikifahamika kwa jina la 
NDOA YANGU, ndania yake yuko mhusika mkuu mwingine 'Jackline Wolper' ambayo kwa maelezo ya Step wanadai filamu hiyo imetengenezwa kwa kiwango cha juu ambapo haiwezi kukopiwa kirahisi na

maharamia wa filamu.Filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi Septemba mnamo tarehe 28 na wapenzi wa msanii huyo aliyetamba sana kwenye ulimwengu wa filamu Tanzania na hata Duniani watakuwa na uhakika wa kumuona staa huyo kwenye filamu hiyo mpya.


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...