Sunday, September 9, 2012

CLOUDS YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA TABORA

Hii ni sehemu ya nje ya kituo hicho cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza kama kinavyoonekana,kituo hicho kipo nje kidogo ya mji wa Tabora,kina jumla ya watoto wapatao 30. 
    


Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini,Mh Suleiman Kumchaya sehemu ya msaada wa vyakula uliotolewa na kampuni hiyo kwa kituo cha ST.Francis kilichopo maeneo ya Ipuli nje kidogo ya mji wa Tabora mjini,anaeshuhudia kulia ni Mlezi wa kituo hicho
 Father Anthony Rajesta pia akipokea msaada huo kwa niaba kutoka kwa mkuu wa Wilaya,Shoto nyuma ya Mkuu wa Wilaya ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini,
Mh Aden Rage ambaye pia alijitolea mipira ya mitano kwa ajili ya michezo ya kituo hicho.


Juunibaadhi ya wasanii waliojitokeza kushiriki katika suala zima la kuisaidia jamii isiyojiweza.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya na pia ni muigizaji wa filamu,Shilole akiwaimbia moja ya wimbo wake watoto wa kituo hicho ambao walionekana kufurahi kutokana na ujio wa wasanii hao.

Hawa ni baathi ya watoto wanaolelewa na kituo hicho wakiwa na baadhi ya walezi wao.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...