Wednesday, September 26, 2012

HAWANDIO WATAKAO SHIRIKI MISS TANZANIA

Warda Frenk katikati akiwa na mshindi mwenzake Anande Raziel upande wa kulia na Lucy Stefano kushoto haowote ni washindi wa Redds Miss kanda ya kaskazini,wote wanatarajiwa kujiunga na kambi ya Redds miss Tanzania.  
Redds miss kanda ya Mashariki 2012,katikati ni Rose Lucas,Irine Veda (kulia) na mshindi watatu Joyce Baluhi,baada yakutangazwa washindi wa shindano hilo lililofanyika Mjini Morogoro Sept 1 2012,Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redds miss Tanzania 2012.
Redds miss Kinondoni Brigit Alfred (katikati),Diana George(kulia)ni mshindi wa pili,Irene David(kushoto)mshindi wa tatu,Brigit pia anashikilia taji la Redds miss Sinza 2012,Irene yeye akishikilia taji la Miss Ubungo 2012
Redds ukanda wa ziwa 2012/13 Eugene Fabian (katikati),kulia kwake ni mshindi wa pili Haappiness Daniel,Kushoto Happiness Rweyemamu,warembo hawa wataingia kambi ya Redds Miss Tanzania 2012.  
Naomi Jones,Caren Elias na Venance Edward  
Malkia wa Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester (katikati), akiwa na mshindi wa pili Flavian Maeda (kushoto), pamoja na Catherine Masumbigana aliyeshika nafasi ya tatu katika kilele cha mashindano hayo, Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Redds miss kanda ya kati,Belinda Mbogo(katikati)akiwa na mshindi wa pili Lightness Michael(kushoto)na aliye twaa nafasi ya tatu Elizabeth Diamond baada ya kumalizika kwa shindano hilo Dodoma.
 Redds miss ilala 2012,Noela Michael akiwa na mshindi wa pili Magdalen Munisi(kulia) na mshindi wa tatu Mary (kushoto)mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Redds Miss ilala 2012.


Jumla ya warembo 30 wanataraji kuingia kambi ya REDDS MISS TANZANIA 2012 wakati wowote baada ya kumalizika kwa mashindano ya Vitongoji, Mikoa, na hatimaye Kanda mwishoni mwa wiki iliyopita.


Kwa mujibu wa mashindano hayo ya Kanda 
ambayo kila Kanda imetoa washindi wa tatu ambao wataziwakilisha Kanda zaoi katika Shindano hilo kubwa na laiana yake.


Warembo hao na Kanda zao wanazotoka ni Redds Miss Kanda ya Kaskazini Warida Frenk, Anande Raziel na Lucy Stefano, Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012 ni  Rose Lucas, Irine Veda na Joyce Baluhi , Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, Diana George Hussein na Irene David.


Kanda nyingine ni Redds Miss Lake zone 2012 Eugene Fabian,Happiness Daniel na Happiness Rweyemamu, Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester, Flavian Maeda na Catherine Masumbigana, Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo, Lightness Michael na Elizabeth Diamond.


Washiriki wengine watakao ingia Kambini ni kutoka kanda ya Redds Miss Ilala 2012, Mary Chizi, Magdalena Munisi na Noela Michael, Redds Kanda Vyuo vya Elimu ya Juu, Virginia Mokiri, Fatma Ramadhani na Fina Revocatus, kanda nyingine ni ya Kutoka Chuo Kikuu Huria ni Zuwena Nassibu na Redds Miss Southern Zone Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward.
Kesho Septemba 26, 2012 Kamati ya Miss Tanzaniaikiongozwa na Mkurugenzi wake Hashim Lundenga kutoka Lino International Agency watakutana na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maeleo majira ya saa 4:00 asubuhi kuzungumzia maandalizi ya Kambi hiyo.


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...