Tuesday, December 11, 2012

UWOYA ATOA KITUKO CHA MWAKA

Kituko hicho kilitokea katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wakati Uwoya alipokuwa akiomba kura mbele ya wasanii wenzake.

Kauli yake hiyo iliwashangaza wengi kwa kuwa Uwoya ni mmoja kati ya wasanii wanaoongoza kwa kuandikwa kwa skendo.
“Hakuna asiyejua jinsi skendo zilivyonichafua, nilipogundua kuwa zinaniharibia maisha nikaachana nazo, sasa ole wao wote wenye tabia za aina hiyo, hakika watanitambua,” alisema na kuzua minong’ono.
Pamoja na minong’ono hiyo, Uwoya alifanikiwa kuwabwaga wapinzani wake Benny Kinyaiya na Lissa Aidan na kuchukua nafasi hiyo.


Nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye hakuwa na mpinzani na Chick Mchoma ‘Chiki’ alichaguliwa kuwa Katibu.
Simon Mwapagata aliwashinda Juma Chikoka na Chuchu Hans katika nafasi ya katibu msaidizi.
Single Mtambalike ‘Richie’ hakuwa na mpinzani katika nafasi ya mweka hazina na Jacqueline Wolper Massawe alimbwaga Cathy Rupia katika nafasi ya mweka hazina msaidizi.

BIG UP UJANA Tz




No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...