Saturday, December 22, 2012

TAJOA;MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAMPA DHAMANA LULU;Msanii Lulu kula Xmas akiwa kwao

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imempa dhamana msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inadhaminika.

Kwa maana hiyo, Lulu sasa atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusudia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...