Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya
Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya
maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila
mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji,
Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili
kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment