Mashabiki wa Simba novemba 5 2012 waliandamana mpaka makao makuu ya club hiyo Msimbazi Kariakoo Dar es salaam wakiwa na mabango mbalimbali yanayomaanisha wamechoka na ishu mbalimbali za club hiyo.
Mabango mengine yalisomeka kwamba mamluki wajirekebishe Simba mmeikuta, mengine Ndugu Kaburu kocha wetu Milovan mchango wake mkubwa bado tunamuhitaji, Kaseja tuachie
Mabango mengine yalisomeka kwamba mamluki wajirekebishe Simba mmeikuta, mengine Ndugu Kaburu kocha wetu Milovan mchango wake mkubwa bado tunamuhitaji, Kaseja tuachie
timu yetu.
Hiyo yote imetokana na Simba kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar novemba 4 2012 Morogoro.
Baada ya kichapo hicho katika msimamo wa ligi kwa timu kongwe jijini Dar es Salaam, YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga Azam FC 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26 ikiwa imebakiza mechi moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 23 ambayo imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar Morogoro.
Milard ayo
No comments:
Post a Comment