Friday, November 30, 2012

JB MPIANA ATUA NCHINI NA KUNDI LA WENGE MUSICA BCBG

Mwanamuziki nguli wa dansi JB Mpiana ametua jijini Dar es Salaam tayari kwa maonesho kadhaa ilikwemo la uzinduzi wa albamu ya Mashujaa Band litakalofanyika ijumaa katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam

Kabla ya onesho hilo la Ijumaa JB Mpiana ambaye amekuja na kundi lake la Wenge BCBG likiwa na wanamuziki wa zamani na wapya leo watafanya makamuzi jijini Arusha kabla ya kwenda Mwanza jumapili

Akizungumza na waandishi wa habari jijini JB Mpiana amewahidi watanzania kufanya shoo ya aina yake akiamini watanzania wengi itakonga nyoyo zao

"Nimefurahia mno kuja Tanzania kwa mara nyingine ikiwa ni pamoja na mapokezi niliyoyapata ambayo yananifanya niahidi kutoa burudani ya nguvu kwa mashabiki watakao hudhuria shoo zake" alisema

Alisema atapiga nyimbo za zamani na mpya katika programu yake ya hapa nchini ili kuwapa radha tofauti mashabiki wa dansi nchini


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...