Wednesday, September 12, 2012

WANAHABARI WAANDAMANA NCHI NZIMA KULANI MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI


Mhariri Mkuu wa Channel Ten, Dinnah Chahali akiwa amezungukwa na waandishi wa habari wakati wa maandamano ya wanahabari jijini Dar es Salaam kupinga kuuawa kwa mwakilishi wa kituo hicho mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

Waziri wa mambo ya Ndani, Dk. Nchimbi nae alivamia hapa na wanahabari wa jijini Dar es Salaam kumkataa na kuamua kuondolewa na vijana wake kwa kuhofia usalama wa ke dhidi ya Camera na Kalamu. 
Kutoka viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam: Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena, akihutubia waandishi wa habari walioandamana kulaani mauaji yaliyofanywa na polisi dhidi ya mwandishi Daudi Mwangosi mkoani Iringa hivi karibuni.
   
Hapa ni Moshi mjini Viongozi wa KPC nao walishiriki vyema Maandamano hayo .
          
       
Napo Moshi Polisi wa usalama barabarani waliamua kubeba jukumu la wanahabari kwa kupiga picha za matukio mbalimbali. Uandishi wa habari ni Mzuri bwana.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...