KOFFII OLOMIDE ASHITAKIWA
Koffi Olomide, ambaye
ni mwanamuziki mashuhuri barani Afrika ameshitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji
wake wa muziki.
Mwanamuziki huyo
alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani
jumatano.
Koffi alikamatwa
kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.
Waandishi wa habari
wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja
kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa
hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati wa kesi hiyo
hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya
mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola
$3,680.
Hakimu alimfahamisha
mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Olomide ni gwiji wa
muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa
"secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake
vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.
No comments:
Post a Comment