Tuesday, November 13, 2012

BEN POL AJIVUNIA USHINDI WA WALTER CHILAMBO

 MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni sukari ya warembo Ben Pol ajivunia ushindi wa Walter Chilambo alioupata katika kinyanganyiro cha Epiq Bongo Star Search 2012 huku akisema kuwa anauwezo wa kufanya naye kazi hata kumuandikia nyimbo ikiwa yeye mwenyewe akiwa tayari kufanya naye kazi.

Alisema kuwa mshindi huyo ameweza kupata ushindi kwa kutumia nyimbo zake ambazo ameziimba kwa umahiri mkubwa na kuonyesha ukomavu katika tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya

Ben Pol alisema kuwa kutokana na kazi yake kuwa nzuri ndio maana wasanii chipukizi wanaingia katika tasnia hiyo huku wakimwangalia yeye katika utendaji wa kazi zake.

"Kwangu mimi ni faraja kubwa sana kuona baadhi ya wasanii chipukizi wanaiga kile ninachokifanya tena wanafanya kwa juhudi kubwa na wengine kuchukua ushindi kwa hali hiyo inaonesha ni jinsi gani ninavyofanya kazi nzuri inayomvutia kila mtu" alisema Ben Pol

Pamoja na hayo Ben Pol alimtaka mshindi huyo kuwa makini katika utendaji wake wa kazi na kuwa na nidhamu ka siraha yake ya mafanikio ili kufika pale anapopakusudia katika tasnia ya muziki

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...