Thursday, November 1, 2012

SIHITAJI KUTANGAZA KIASI GANI NALIPWA KWENYE KILA FILAMU BALI KIWANGO CHANGU NI JIBU TOSHA” – ZAMZAM…!!

 MSANII wa filamu za kibongo asiye na matukio ya ajabu Zamzam Salim ‘Zamzam’, amedai kuwa haoni sababu ya kutangaza anataka kulipwa kiasi gani katika kila filamu kwani anaamini ubora wa kiwango chake ndio jibu sahihi kwa waandaaji kwani hataki ufuata mkumbo kama wale ambao kila siku wanajitangaza wakati ukitazama viwango vyao si vya kutisha.

Sasa umeibuka mtindo kwa kila msanii anayejiona staa kutangaza dau analotaka kulipwa katika filamu wakati wengine hajawafikia hatua hata ya kuitwa ‘Professional Actor/Actress’ au kufikia kiwango cha kujulikana hata Afrika Mashariki.
Alisema kuwa wasanii wanaotangaza kutaka kulipwa kiasi fulani cha pesa ni wale ambao wanajiona mastaa kwa sababu ya kutokea kila siku kwenye vyombo vya habari huku wengine wakitokea kwa mambo ya ajabu basi tayari wanajiweka kwenye ubora wa hali ya juu.
Zam katika pozi

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...