Na vihi ndivyo ilivyokua
Jitu moja ambalo halikufahamika jina lilimtapeli mfanya biashara kwakumpa makaratasi,HAPA akipatiwa kichapo na wanachi wenye asira kali.
Akiwa na wenzake huku wakitumia usafiri wa gari aina ya Noah yenye namba za usajili wa Uganda (bahati mbaya hazikunukuliwa) Tapeli hilo (pichani) mara baada ya kukamilisha kufanya biashara na tajiri huyo kuwapatia mali, Matapeli hayo yaliondoka eneo la biashara huku wakimwacha tapeli mwenzao aliyepichani hatua chache toka eneo la tukio ili asome harakati za mfanya biashara huyo pindi atakapostukia kuwa kapewa makaratasi ya kimazingaombwe na si za madolali kama halali ya malipo.
Waliposepa wazeeya, yule Mfanyabiashara maarufu akagutukia mchezo ingawa alikuwa kisha chelewa kwani matapeli wengine walikwisha timua eneo la unoko.
Angaza huku na kule ...mara nkabaaaaa jicho likamnasa mmoja aliyewaona nao... mfanyabiashara akakusanya washirika wenzake ... mara tip ... tapeli aliyekuwa akichungulia msala akanaswa na kuanza kuchezeshwa kichapo.
Ni daftari lililo katwa kiufundi saiz ya dola za kimarekani
Wengi wafanyabiashara hususani wa samaki na wavuvi wamekwisha lizwa na matapeli hao jijini hapa wakibamizwa na biashara za dhahabu feki, almasi feki na mitindo mingine ya kubadilisha fedha za madafu kwa dola za Kimarekani.
No comments:
Post a Comment