Monday, October 8, 2012

AFRICA MAGIC KWA KUSHIRIKIANA NA MULTICHOICE YAANDAA TUZO KWA WAIGIZAJI NA WATENGENEZAJI BORA WA FILAMU BARANI AFRIKA.

Pichani Juu na Chini ni Meneja wa MNET Ukanda wa Afrika Mashariki Bi. Risper Muthamia wakati wa kutangaza rasmi kutolewa kwa Africa Magic Viewers Choices Awards (AMVCA), ambapo amesema zitawashirikisha Wasanii, Waandaji na Waandishi wa Filamu kutoka Barani Afrika zitakazofanyika Lagos nchini Nigeria tarehe 9 Machi 2013.

Bi. Risper Muthamia amesema kuwa Filamu zote zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni na mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) zinaweza kuwasilishwa kuwania tuzo hizo iwapo zilitengenezwa na kurushwa hewani au kuonyeshwa hadharani katika kipindi cha kati ya May 1, 2011 hadi April 30, 2012.
Aidha amefafanua kuwa Filamu au vipindi vitakavyoshiriki katika tuzo hizo viwe ni katika lugha ama ya Kiingereza, Hausa (Nigeria), Swahili au Yoruba na kusisitiza kuwa hakuna Lugha nyingine itakayokubalika.

Ameongeza kuwa Filamu na Sinema zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni zinapaswa kuwa na urefu wa kati ya Dakika 60 mpaka 90 wakati Mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) ni kwa muda wa dakika 30 mpaka 60. Wasanii wamekumbushwa kuwa ili kuweza kushiriki katika tuzo hizo wanapaswa kuwasilisha nakala 6 za DVD za filamu zao. 


Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza katika semina fupi ya wadau wa tasnia ya Filamu nchini pamoja na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa wasanii watakaopelekea kazi zao wahakikishe kuwa sio za kuiga na zina hati halali ya kusajiliwa na COSOTA.



  Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akiteta jambo na mmoja wa washiriki wa semina hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufafanua vigezo vitakavyotumika wakati Africa Magic Viewers Awards (AMVCA) zinazotarajiwa kufanyika March 9, 2013 Lagos Nigeria.
 

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Bw. Jai (wa pili kushoto) ambao ni wasambazaji wa filamu nchini akizungumza na maafisa wa kampuni ya Multichoice. 
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini waliohudhu8ria semina fupi iliyohusiana na Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA). Kutoka kushoto ni Msanii Sajuki akiwa amembatana na mkewe na msanii nguli Dkt. Cheni.
 


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...